Hivi karibuni nilikuwa Dar es salaam kwa likizo fupi, nikashangaa mtaani kwetu, msiniulize maeneo gani, nilikuta wakaazi wengi waliokuwa wakifuga kuku wa mayai au wa nyama wamebadili biashara na sasa wanafuga ndege aina ya Kware na wanauza mayai yake kam njugu.
Nilipodadisi niliambiwa yanatumiwa na waathirika wa ugnjwa wa UKIMWI maana wameambiwa na wataalmu wetu kwamba mayai ya Kware yanatibu UKIMWI.
Nilishangaa zaidi kusiki eti dozi yake ni mayai matano kwa siku kila siku na baada ya kutumia kwa miezi mitatu mgonjwa anapona kabisa. Si hivyo tu nikasikia madai mengine kwamba hayo mayai ya Kware yanatibu pia ugonjwa wa Kansa.
Napenda kuwausia Watanzania wenzangu kwamba dawa ni kuacha ngono, mayai ya Kware hayatibu UKIMWI
Loading...
Post a Comment