Wakati mchakato wa CCM kutafuta mgombea Urais ukitarajiwa kuanza mwezi ujao, imebainika kuwa kuna mkakati wa kuyapiga chini makundi ya makada wanaosaka urais ili kupata mgombea ayakayekinusuru chama hicho katika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.
CCM imekuwa ikipata wakati mgumu kila mwanacma wake anapomaliza vipindi vyake viwili vya urais, na safari hii kazi ya kumpata mrithi wa Rais Jakaya Kikwete ambaye amepata urais mwaka 2005 inaonekana kuwa ngumu zaidi na huenda ikasababisha chama hicho kupunguzwa nguvu zaidi iwapo haitafanya uamuzi unaokubalika na makundi yote ya Urais.
Makundi makubwa yanayolengwa na mkakati huo wa kuyapiga panga, ni ya makada wanaoonekana kuwa na nguvu na ushawishi mkubwa ambayo kambi zao zimekuwa zikipambana vikali kwenye vita ya chini kwa chini ya Urais.
Makundi hayo ni lile linalomuunga mkono Lowassa na linalomuunga mkonoMembe,watu wanauwaunga mkono makada hao wamekuwa wakipishana mikoani kuweka mambo sawa kwa vigogo hao, hali ambayo inaonekana kuwatisha CCM kiasi cha kuchelewa kutangaza kwa mchakato wa Urais ndani ya chama hicho.
Tayari makada hao na wenzao wamepwa onyo kali inayowazuia kuwania nafasi yoyote kwa kipindi cha miezi 12 na adhabu hiyo ilikuwa imalizike Februari mwaka mwaka huu lakini imeongezwa muda kutokana na kamati ya maadili kuendelea na uchunguzi.
HABARILEO
Wakati ajali za barabarani zikiendelea kumaliza nguvu kazi ya Taifa na kuumiza vichwa vya Watanzania kuhusu suluhisho la ajali hizo, imefahamika moja ya tatizo sugu ni kukosekana kwa madereva wenye taaluma stahiki, ingawa wana leseni.
Wiki hii peke yake, ajali tatu za mabasi zilizotokea Mbeya, Morogoro na maeneo yaMwanza, zimesababisha vifo vya watu 40 ndani ya siku sita.
Tayari Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, ametoa takwimu za vifo vilivyotokana na ajali za barabarani kati ya Januari Mosi mwaka huu hadi Aprili 12, sawa na siku 102 vifo 969.
Kwa upande wa usafiri wa kutumia pikipiki za magurudumu mawili (bodaboda), Kamanda Mpinga ameeleza kuwa kati ya Januari na Machi, sawa na siku 90 madereva wa bodaboda ambao Serikali ilishakiri kuwa wengi hawana leseni, wamesababisha vifo vya watu 220.
Akizungumza na gazeti hili wiki hii, mmoja wa wataalamu wa mambo ya usafirishaji nchini, alisema mabasi ya kusafirisha abiria nchini, ni mengi kuliko idadi ya madereva wenye taaluma ya kuendesha abiria.
Mazingira hayo ni sawa na usafiri wa bodaboda, ambao nao unakabiliwa na tatizo kubwa na pikipiki nyingi zilizosajiliwa, kuliko idadi ya madereva wake waliopatiwa leseni.
“Mimi nina uhakika kabisa ajali hizi zina uhusiano mkubwa na mafunzo kwa madereva, kwa kuwa kama dereva angekuwa anapona katika ajali, tungesema amepata mafunzo stahiki, lakini wengi wanakufa kwakuwa hawana mbinu za kupambana na ajali,” alisema.
Alisema ni dhahiri kuwa madereva wa Tanzania hawana ujuzi wa kutumia vyombo hivyo na kufafanua kuwa, vyombo wanavyoendesha vinajulika vinaua, ndio maana katika mafunzo madereva lazima wapewe mbinu ya kujilinda kama inavyofanyika katika nchi nyingine.
Mtaalamu huyo alihoji iweje marubani wa ndege binafsi, zinazobeba abiria wanne hadi sita, wapelekwe katika mafunzo kila baada ya miaka minne, lakini kwa madereva wanaobeba abiria zaidi ya 65, wanakataa kupelekwa mafunzo baada ya miaka mitatu na kuongeza kuwa hapo kuna tatizo lazima liangaliwe.
Alisema madereva wanapaswa kuelimishwa kuwa mafunzo hayo, ndio mwanzo wa kuandaa kanuni za mafunzo kwa madereva, ili watambulike rasmi kama walivyo marubani na manahodha.
Uzoefu nchi nyingine Mtaalamu huyo alisema duniani kote udereva hususan wa abiria, ni kada ya juu inayolipwa mshahara mkubwa, huku mafunzo yake yakiwa magumu na huchukua muda mrefu.
Alitoa mfano wa nchi ya Uingereza, ambako mtihani hufanyika kwa kutumia mtandao wa kompyuta, ambapo kama dereva mtarajiwa akifaulu kwa kupata zaidi la asilimia 70, cheti kinajiprinti chenyewe.
Alisema katika mafunzo hayo, hakuna kujuana bali kompyuta tu zinafanya kazi na hivyo ufaulu wake na kupata cheti au leseni ni halali, kuliko kufanya mtihani kwa kujuana na kupeana leseni.
Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, mitihani hiyo katika baadhi ya nchi ikiwemo Afrika Kusini na Japan, hata leseni ya gari dogo, dereva lazima afanye mtihani kabla ya kupata leseni.
HABARILEO
Serikali imerejesha mafunzo ya madereva kila baada ya miaka mitatu wakati wa kumalizika kwa muda wa leseni zao, huku ikifafanua kuwa elimu watakayoipata ina umuhimu katika kazi zao, kutokana na mabadiliko mbalimbali yanayotokea katika sekta hiyo.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga, alitangaza uamuzi huo wa Serikali jana katika mkutano kati yake na viongozi wa madereva wa mabasi nchini.
Mkutano huo umefanyika kama ilivyoahidiwa na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, wakati alipokuwa akijitahidi kumaliza mgomo wa madereva uliofanyika Aprili 10 mwaka huu, wakati walipokuwa wakipinga pamoja na mambo mengine, sharti la kwenda shule ili kupata leseni mpya.
Madereva hao walitaka Serikali ifanyie marekebisho Sheria ya Usalama Barabarani, kwa kuondoa kipengele kinachowataka madereva kwenda Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) kwa mafunzo ya muda mfupi kila wakati leseni zao zinapoisha, ili kupata sifa ya kupata leseni nyingine.
Sababu ya kupinga kupata mafunzo, ilidaiwa kuwa utaratibu huo uliotangazwa Machi 30, mwaka huu, ulianzishwa bila kushirikisha madereva katika kuuandaa.
Pia walipinga kutakiwa kujilipia gharama za shule hiyo ambazo walidai ni Sh 560,000 kwa magari ya kawaida na Sh 200,000 kwa magari ya abiria.
Sababu nyingine iliyochangia wapinge shule hiyo, walidai ni kukosekana kwa mikataba ya ajira, inayoweza kuwahakikishia kulindwa kwa kazi zao hadi wanapomaliza mafunzo.
Madai mengine yaliyokuwa nje ya shule hiyo, madereva hao walitaka kuondolewa kwa faini ya Sh 300,000 kwa kila kosa la barabarani na kuitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchikavu (SUMATRA), kuhakiki uhalisia wa dereva anayeandikishwa na mmiliki wa chombo husika.
Majibu ya Serikali Mahanga aliyekuwa Mwenyekiti wa kikao hicho, alisoma tamko la Serikali lililoeleza kuwa pamoja na kurejesha mafunzo hayo, utekelezaji wake hautafanyika mara moja kwa kuwa Kanuni zake hazijakamilika.
“Tangazo hili (la kwenda shule) limetolewa kwa kuzingatia umuhimu wa mafunzo kazini kwa wafanyakazi na madereva kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine,” Mahanga.
Alisisitiza kuwa baada ya miaka mitatu ya leseni, dereva atatakiwa kupata mafunzo mafupi, ambayo ni kati ya siku tatu hadi saba na atakayegharimia mafunzo hayo ni mwajiri, si mfanyakazi na ni katika chuo chochote kinachotambulika.
Akifafanua, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Mwamini Malemialiyekuwepo katika mkutano huo, alisema mitaala ya mafunzo hayo bado inaandaliwa, hivyo si rahisi Kanuni hiyo kuanza kutekelezwa mwaka huu hata kama zitakamilika.
Kuhusu mikataba ya ajira ambayo ililalamikiwa mno na madereva wakati wa mgomo, Mahanga alisema Serikali itapitia upya mikataba hiyo ili kuhakikisha mambo yote muhimu yanazingatiwa.
Akiongezea hoja katika suala la mikataba, Malemi alisema ni lazima mikataba iwe imekamilika kabla ya kuanza kutumika kwa kanuni ya kwenda shule, ili ioneshe wajibu wa mwajiri katika kumsomesha mfanyakazi.
Kuhusu kauli iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Suleiman Kova ya kuondoa tochi za kupima mwendo kasi barabarani, Mahanga alisema matumizi ya tochi zinazotumika kupima mwendo kasi na ratiba ni sehemu ya utekelezaji wa Sheria za Usalama Barabarani.
MTANZANIA
Raia wa Tanzania wanaoishi Afrika Kusini sasa wanadaiwa kushika silaha tayari kwa mapambo dhidi ya vikundi vya raia wa Taifa hilo vinavyoshambulia wahamiaji wa Kiafrika.
Taarifa zilizolifikia Gazeti hilo kutoka kwa Watanzania hao imeeleza hatua hiyo imefikiwa baada ya kupatikana kwa taarifa zinazodai kuwa wenzao wawili wameuawa katika machafuko ya jiji la Durban ambayo chanzo chake ni mashambulizi yanayofanywa na raia wan chi hiyo dhidi ya wageni.
Mmoja wa Watanzania anayeishi Cape Town, Pius Mbawala alieleza kuwa taarifa za mauaji ya wenzao zimewasikitisha sana na kwamba hadi sasa hakuna kiongozi yoyote wa ubalozi wa Tanzania aliyewasiliama nao ili kujua hali za usalama wao tofauti na balozi za nchi nyingine.
Mbalawa alisema kwa muda mrefu sasa maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini humo wamekuwa na uhusiano wenye shaka na Watanzania walioko huko tofauti na wanavyopaswa kujua ukazi wao kwenye Taifa hilo.
Alisema Raia wa Tanzania wanaoishi nchini humo wamejiunga katika makundi madogo madogo kulingana na maeneo wanayoishi kwa ajili ya kujilinda wenyewe na kila kundi hivi sasa limejihami kwa silaha.
MTANZANIA
Umoja wa madereva nchini umesema umemwandikia barua Waziri mkuu Mizengo Pinda kulalamikia hatua ya Serikali kutoyashughulikia madai yao.
Pia kama hali hiyo itaendelea hivyo wametishia kugoma tena kufanya mgomo mwingine.
Katibu wa Umoja huo Abdallah Lubala alisema kilichofanyika walipokutana na na Naibu Waziri wa Kazi na ajira Dk.Makongoro Mahanga ni siasa.
“Serikali inatufanyia siasa kwa kuwa tulipofika badala ya kukutana na Waziri ili kujadili suala letu tuliishia kusomewa barua na Mahanga inayonukuu kikao cha April 9 tulipokutana na Waziri, sasa hapo tunajiuliza kama walikuwa na majibu kama haya kwa nini walishindwa kuyasoma?” Lubala.
Alisema juzi ikiwa ni siku moja baada ya kukutana na Mahanga kilifanyika kikao na wamiliki wa magari kilichozidisha shaka yao kwa kuwa hawana imani nacho kutokana na wao ndio waliomba mkutano huo.
Katika barua hiyo ambayo ina kichwa cha hbabari kuhusu tamko la Serikali juu ya hoja za madereva zilizotolewa katika kikao kati ya waziri wa kazi Kabaka na viongozi hao, Serikali ilisema itachukua hatua ikiwemo ya kupitia upya mikataba ya ajira zao ili kuhakikisha mambo muhimu kama mishahara,malipo ya saa za ziada,likizo na michango ya hifadhi yanatekelezwa.
MWANANCHI
Mmoja wa majeruhi wa ajali iliyoua watu 19, Mariam Manfredy (28) aliyevunjika mguu wa kushoto, anasimulia ajali hiyo na kusema chanzo ni mwendo kasi na kuungua kwa breki.
Gari hilo lilikuwa ‘limeshona’ abiria, lilikuwa likitoka jijini Mbeya kwenda Kiwira wilayani Rungwe kabla ya kuanguka eneo la Mto Kiwira na kuua watu 18 palepale na mmoja alifia Hospitali ya Igogwe huku wengine watatu wakijeruhiwa.
Mariam aliyelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya (MRH), alisema alipanda basi hilo katika Kijiji cha Simambwe akienda Kiwira kununua bidhaa za biashara.
“Tulipofika Kijiji cha Ndaga, magurudumu yalianza kutoa cheche na moshi jambo lililomfanya kondakta kuteremka na kuzima kwa maji na kwamba wengi walisema breki zimeungua kwa kuwa kulikuwa na harufu kali ya kitu kinachoungua.
“Baada ya kuzima moto kwenye matairi hayo, dereva aliendelea na safari kwa kasi na ndipo basi lilipoongeza kasi kubwa ambayo iliwafanya abiria wote wapige kelele kumtaka dereva apunguze mwendo, lakini yeye hakusema lolote.
“Mimi nilikuwa nimesimama mlangoni na kondakta wa gari hilo na hata ajali hiyo ilipotokea sikuiona bali alijikuta nikiwa kwenye maji hadi nilipookolewa na wasamaria wema.
“Nilipotokea ni kama Mungu tu hakutaka nife…gari ilipinduka vibaya na wengi wamekufa, jamaa zangu na wengi tulikuwa tunakwenda kununua bidhaa kwa ajili ya biashara zetu.”
Katika ajali hiyo watu 19 walipoteza maisha na hadi jana maiti 15 kati ya 18 zikichukuliwa na ndugu zao.
Hospitali ya Rufaa ya Mbeya ilifurika umati wa watu waliokuja kushuhudia na kutambua majeruhi pamoja na kuchukua miili ya jamaa zao.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Aminiel Ngamuo alisema baada ya ajali ndugu wa marehemu walimimika juzi jioni kuzitambua na walifanikiwa kuwatambua ndugu zao huku maiti tatu za wanaume zikiwa zimebaki hadi jana mchana.
Hata hivyo Dk Ngamuo alishindwa kutaja majina ya waliotambuliwa akisema majina yalifungiwa kwenye ofisi zingine.
Maeneo mengi ya mkoa wa Mbeya yalikuwa na vilio hasa katika maeneo ya Iyunga, Nzowe, Uyole na Mwanjelwa ambako abiria hao walitokea.
MWANANCHI
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta amesema anasubiri kukamilika kwa utaratibu wa CCM wa kugombea urais ili aingie rasmi kwenye mbio hizo kwa kuwa anaridhika na mambo matatu ambayo anasema yanamfanya ashawishike kugombea nafasi hiyo ya juu katika siasa nchini.
Sitta, mwanasiasa mkongwe na Spika wa Bunge la Tisa, ni mmoja kati ya makada wa chama hicho tawala wanaotarajiwa kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya CCM kugombea urais kumrithi Jakaya Kikwete, ambaye anamaliza vipindi vyake viwili vya urais Oktoba mwaka huu.
Akizungumza na Mwananchi mwishoni mwa wiki, Sitta alisema zaidi ya mambo hayo matatu, anaamini ana ushawishi mkubwa na Watanzania wengi wanamwamini katika utendaji kazi wake.
“Nina mengi nimefanya kutokana na historia yangu ya kiutendaji na ndiyo nitakayoitumia kama mtaji utakaonibeba kwenye harakati hizi,” alisema.
Sitta, ambaye alikuwa mwenyekiti wa Bunge la Katiba, alitaja mambo hayo matatu ambayo ni mtaji wake kuwa ni uendeshaji wake wa chombo hicho cha kuandika Katiba, uendeshaji wake wa Bunge na uzoefu wake wa muda mrefu kwenye nafasi mbalimbali alizowahi kushika.
Sitta, ambaye alikuwa mwenyekiti wa Bunge la Katiba, alitaja mambo hayo matatu ambayo ni mtaji wake kuwa ni uendeshaji wake wa chombo hicho cha kuandika Katiba, uendeshaji wake wa Bunge na uzoefu wake wa muda mrefu kwenye nafasi mbalimbali alizowahi kushika.
“Niliendesha Bunge la Katiba kwa mafanikio na hata kupatikana kwa Katiba Inayopendekezwa,” Sitta.
“Watanzania wataangalia wenyewe historia yangu kwani mimi ndiye mwenyekiti niliyefanikisha kutimiza ndoto za Watanzania kupata Katiba mpya kupitia Bunge Maalumu la Katiba, haikuwa rahisi katika tukio hilo,” alisema.
Hata hivyo, Bunge la Katiba halikuisha kwa maridhiano baada ya wajumbe kutoka vyama vinne vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD kususia vikao kwa madai kuwa chombo hicho kiliweka pembeni Rasimu ya Katiba iliyokuwa na maoni ya wananchi.
Juhudi za Sitta kuwarejesha vikaoni ziligonga mwamba, lakini mchakato ukaendelea hadi Katiba Inayopendekezwa ilipopatikana.
Sitta alisema mtaji wake mwingine katika mbio za urais ni na kuimarisha demokrasia ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano.
“Mimi ndiye niliyebadilisha Bunge baada ya kubadilisha kanuni za Bunge mwaka 2007, ambazo zilitoa uhuru, haki na usawa kwa wabunge wote bila kujali wapinzani,”alijigamba.
NIPASHE
Mwanamke mmoja mkazi wa Mabibo mwisho, Jijini Dar es slaam anadaiwa kuanzisha danguro la wasichana na kuendesha biashara ya ngono ikiwamo ya jinsia moja.
Mwanamke huyo anayefahamika kwa jina la mama Uzuri, anadaiwa kuwachukua wasichana hao kutoka vijijini kwa kuwadanganya kuwa anakwenda kuwatafutia kazi mjini.
Inadaiwa kuwa fedha anazopata kutokana na biashara hiyo huzitumia kama gharama ya kuwatunza wasichana hao.
Wasichana hao kwa nyakati tofauti walidai mwanamke huyo aliwachukua kijijini kwa lengo la akuwatafutia ajira za ndani na wamesema wanaume wengi wamekuwa wakiwalazimisha kufanya mepenzi bila kinga kwa madai kunawanyima starehe.
Walisema mwanzo walipoanza biashara hiyo walipata ugumu lakinikadri siku zilizvyokuwa zinakwenda waliizoea.
Gharama za biashara hiyo zinatofautiana kutokana na kiwango cha mteja lakini kwa wale wanaofanyiwa tendo kinyume na maumbile wateja hutozwa 20,000 na kawaida 5,000 hadi 10,000 kwa mara moja.
NIPASHE
Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma, limesema limeshawasilisha ripoti yake kwa Rais Jakaya Kikwete, baada ya kumaliza kazi ya kuwahoji viongozi waliokumbwa na kashfa yaTegeta Escrow.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maandili ya Baraza hilo, Jaji Mstaafu, Salome Kaganda, katika mahojiano maalum juzi alisema kuwa tayari Baraza lake limeshawasilisha ripoti hiyo kwa Rais na kinachosubiriwa ni majibu.
Waliohojiwa na Baraza hilo ni aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, ambaye alipewa mgawo wa Sh. bilioni 1.6 kutoka kwa Mmiliki wa Kampuni ya VIP Engineering and Marketing, James Rugemalira.
Wengine ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, ambaye alichotewa Sh. million 40 katika mgawo huo.
Katika sakata hilo pia, Afisa wa Ikulu, Shabani Gurumo, alihojiwa baada ya kudaiwa kupokea Sh. milioni 80.
“Tayari nimeshaiwasilisha ripoti nasubiri majibu ila sikumbuki terehe niliyoipeleka,” Jaji Kaganda.
Mwenyekiti wa Baraza hilo, Jaji Mstaafu Hamis Msumi, awali alipoulizwa kuhusu hatma ya waliohojiwa, alisema, ameshamaliza kazi yake na kuiwasilisha kwa Kamishna ili ipelekwe kwa Rais.
Balozi Ombeni Sefue ambaye alisema ripoti hiyo itapitiwa kwa umakini ili kujua hatua zitakazochukuliwa.
Vigogo hao ni Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge, Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita), Philip Saliboko na Naibu Kamishna Upelelezi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Loicy Appollo.
Chenge anadaiwa wakati akiwa Mwanasheria Mkuu wa serikali mwaka 1995, aliishauri serikali kuingia mkataba wa miaka 20 na IPTL.
Na baada ya kustaafu, aliingia mkataba kuwa mshauri wa kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited iliyokuwa na hisa asilimia 30 kwenye kampuni ya IPTL.
Katika mgawo wa fedha za Tegeta Escrow, Chenge alipokea Sh. bilioni 1.6, ikiwa ni sehemu ya fedha zilizochotwa katika akaunti hiyo iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
NIPASHE
Kitengo cha moyo hospitali ya Taifa Muhimbili kinakabiliwa na upungufu wa madaktari 24 wa upasuaji hali inayochangia upasuaji wa wagonjwa kushuka kutoka 16 hadi wawili kwa siku.
Mkuu wa kitengo cha moyo Prof. Janabi Mohamed alisema kuwa magonjwa ya moyo yanaongezeka kutokana na kukua kwa uchumi hali inayosababisha wananchi kutofanya mazoezi, kula vyakula vyenye mafuta yanayogeuka kuwa sumu na kushindwa kuchujwa na damu kuwa nzito.
Alisema hali hiyo inasababisha mishipa kuwa mizito na matibabu yake ni upasuaji.
Alisema kitengo hicho kimeshafanya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa 453 tangu kianze miaka miwili iliyopita.
Alisema wagonjwa wengi wa moyo wanapoteza maisha kutokana na kukosa huduma kunakochangiwa na umbali wa kuwafikia wataalam wa moyo.
“Hapa tuna changamoto ya madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa muda wa huu wako wane, kuna upungufu wa madaktari 24, ambapo madaktari 12 ni wa kuzibua mishipa na wengine 12 ni upasuaji wa moyo” Mohamed
Post a Comment