Headlines zenye uzito mkubwa Magazetini leo April 16 2015, iko ya Jeshi la Polisi Morogoro linawashikilia watu 10 waliokamatwa Msikitini wakiwa na vitu mbalimbali ikiwemo milipuko, Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar, Prof. Kitila Mkumbo amesema tatizo la ajira limechangia ukosefu wa maarifa, Waziri Lazaro Nyalandu ameendelea na zoezi la kupambana na majangili, kuna stori ya mume na mke kuhukumiwa kifungo cha miaka ishirini kwa kukutwa na dawa za kulevya.
Nauli za mabasi mikoani zimeshuka lakini SUMATRA imesema haiwezi kupunguza nauli kwa usafiri wa mijini, simu maalum kutumika kuwakamata ‘madereva feki’ TZ, Mbunge wa John Mnyika ameitaka Serikali kulipa uzito tatizo la kukithiri kwa ajali TZ, Serikali imepunguza idadi ya masomo kutoka saba hadi matatu kwa darasa la kwanza na la pili.. imeandikwa pia kuhusu kuagwa kwa miili ya watu 8 waliofariki kwa kupigwa na radi.
Kuna mahojiano pia na Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Gillian Ngewe ambae ametolea ufafanuzi zoezi la kutumia simu ya mkononi ili kutambua madereva TZ.
Post a Comment