28 Aprili 2015 Imebadilishwa mwisho saa 13:19 GMT
Waandamanaji nchini Burundi wameingia mitaani katika siku ya tatu sasa kwa hasira baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuamua kugombea nafasi hiyo tena kwa muhula wa tatu.
Wanaharakati wanasema takriban watu sita wameuawa katika makabiliano huku polisi wakitumia mabomu ya machozi na risasi za moto kutawanya watu.
Kiongozi wa wanaharakati wa haki za binadamu Pierre Claver Mbonimpa amekamatwa.
Na Rais wa zamani Pierre Buyoya aliyehusika katika mchakato wa amani uliomaliza mgogoro wa kikabila zaidi ya muongo mmoja uliopita ameonya kuwa Burundi inaweza kurejea tena katika vita.
Mwandishi wetu Robert Kiptoo yuko mjini Bunjumbura.
Filed Under:
matukio
on Friday, 1 May 2015
Post a Comment