Muda huu katika kukakiribishwa na kukabidhiwa kadi MH.LOWASSA ndani ya CHADEMA ,ameulizwa swali moja kuwa
Swali: Mh. Edward Lowassa unazungumiaje kuhusu kashfa ya Richmond?
Majibu Lowassa: Nipende tu kusema mimi kama waziri mkuu kwa kawaida ya
sheria huwa ninaletewa mkataba muda wa mwisho kuupitia na kuupitisha
huwa sihusiki na kuandaa mikataba,mwenye mamlaka ni waziri husika,hivyo
baada ya kuletewa mkataba husika wa Richmond niliupitia na kiukweli
niliuwekea shaka kwa sababu nilishawahi kuwa waziri wizara ya maji nina
uzoefu na kuandaa mikataba,nilishauri mkataba huo uvunjwe lakini waziri
wa nishati akawasiliana na "NGAZI YA JUU"na kulazimishwa kuupitisha
mkataba huo.
Baada ya kugundulika kuwa mkataba huo ulikuwa na mapungufu mengi,
"NILICHUKUA MAAMUZI MAGUMU KWA AJILI YA SERIKALI,na kubeba mzigo wote
ndio maana hadi leo wanasema mimi ni FISADI WA RICHMOND,nipende kumaliza
kwa kusema kwamba MWENYE USHAHIDI WA RICHMOND AENDE MAHAKAMANI
AKANISHTAKI.
Loading...
Post a Comment