Leo nitazungumzia mambo gani ya msingi ambayo mpenzi unapaswa kufanya
baada yakutengana au kutendwa jambo lisilomfurahisha na mpenzi wake.
Kupishana lugha na kusababisha malumbano kati ya wapenzi ni jambo la
kawaida kama wanadamu, kwani huombana msamaha na kusameheana.
Wapenzi wengi wamekuwa wakilumbana na wakati mwingine wamekuwa
wakitoleana siri zao za ndani kutokana na mhemko wa asira kati yao na
kufanya penzi lao kuwa shubiri au kutodumu.
Mbaya zaidi ni pale
wapenzi hawa wanapotengana, wahajitathimini kujua wapi walijikwaa ili
kutorudia makosa ili kujiepusha na kasumba ya kuachwa au kuacha mara kwa
mara. Kutokana na kutojitathimini huko, utashangaa katika kipindi
kifupi mmoja wao ana mpenzi mwingine!
Hii yote ni kutokana na wengi wa wapenzi kutojua mambo ya msingi ya kuzingatia wakati wanapokwazana au kutengana.
Leo katika kona yetu, nitazungumzia mambo matatu ya msingi ambayo mpenzi unapaswa kutafakari baada ya kuachana na mpenzi wako.
Jambo la kwanza, mpenzi unachopaswa kufanya baada ya kuachana na mpenzi wako ni kujiuliza kwanini ulimpenda?
Unapaswa kujiuliza hivyo kwa sababu hadi kufikia kuwa wapenzi
mmechunguzana mambo mengi ambayo kwa hayo yaliwafanya kuaminina na
kufikia hatima ya kuwa wapenzi, wachumba au kufunga pingu za maisha
(yaani kuishi kama mke na mume).
Wakati unapojiuliza kwanini
ulipendana hadi kuwa wapenzi, lazima urudishe mawazo yako nyuma kwa
kukumbuka mazuri ambayo mmefanyiana, lakini usiruhusu kukumbuka mabaya
yaliyojiri katika penzi lenu.
Kukumbuka mazuri kunakufanya
kisaikolojia kutafakari zaidi na kwa mwanadamu anayetambua umuhimu wa
kusamehe lazima huruma inayoambatana na chozi kujitokeza hapo.
Kama hiyo haitoshi, kujiuliza kwanini ulimpenda na kukumbuka mazuri ya
nyuma ni ishara kwamba huyo alikuwa mpenzi wako mliyependana, na hivyo
lazima `mtima wako’ udunde kidogo pindi litakapokuja swali
`automatikale’ kwamba je ninapoachana na huyu, nitampata mwingine
atakayenifanyia mazuri, makubwa vile? Na hapo lazima mtima wa
kurudisha mahusiana unapoanzia kwa wapenzi waliofundwa!
Kwa
kubali kuanzisha mahusiano ni kiashiria kuwa mlikuwa mnapendana na
katika hali ya ubinadamu kuhitilafiana ni jambo la kawaida, lazima
msameheane na daima kukumbuka mema yaliyojiri katika penzi lenu.
Kwa hiyo katika mazingira mengine unapoupa mtima wako nafasi ya kiburi
cha kutosamehe hujenga saikolojia ya kiburi na kawaida ya kiburi
hujijenga kama tabia na mwishowe tabia ya mpenzi wa aina hiyo ni kuwa na
wapenzi wasiodumu sawa na maji ndani ya pakacha!
Kwa hiyo
wewe unakuwa ni mtu wa hivyo, hata mtoto anayeanza kutambua jua na mwezi
atafahamu tabia zako, vivyo hivyo thamani yako husinyaa kama ua
jangwani.
Baada ya kufahamu kwanini ulimpenda hatua ya pili unayopaswa kuchukwa sasa ni kujiliza kwanini mmetengana wakati mlipendana?
Epuka kukubaliana na msemo wa kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na
mwisho; kwani kwa kuamini hivyo hata ukiingia ndani ya ndoa msemo huo
utakutesa sana na hautadumu katika ndoa kwani utakosa uvumilivu.
Hakuna wapenzi wanaotengana pasipo sababu ya msingi, kaa chini ukiwa
peke yako ukiwa umejipumzisha kitandani au kaa kwenye kijistuli chako,
kochi, mkeka, au sofa lako pale sebuleni, ila saikolojia ya tafakari
nzuri ni kitandani chumbani mwako, hakikisha hakuna kelele halafu
jiulize maswali manne ya msingi: Kwanini mmeachana? Kulikuwa na
mapungufu gani? Nani anapaswa kulaumiwa? Nani alikuwa mkorofi?
Ndani hayo unapaswa ujiulize tena ,je nimemtendea haki mpenzi wangu?
Kama ni ndiyo kwanini kaniacha na kama sio unachopaswa kuangalia
uwezekano wa kumfuata na kumuomba msamaha kama ni muelewa atakusamahe na
kama sivyo basi unapaswa kuwa makini kwa mpenzi wako mpya.
Lakini inashauriwa kutumia njia washauri mahiri, wanasaikolojia wa
mapenzi, wazee na hata ikiwezekana kutumia watu mahiri katika imani
kabla ya uamuzi wa kuwa na mpenzi mwingine.
Kwa kujiuliza
kwanini mmetenganga itakusaidi kujua sababu za kutengana na baada ya
hapo kama ukiamua kuingia kwenye uhusiano mpya itaweza kuepuka kufanya
makosa kama uliyoyafanya mwanzo na hivyo itapelekea furaha kwenye penzi
lako jipya.
Kabla ya kuchukwa hatua ya kuanzisha uhusiano
mapya unashauriwa kutojihusisha katika swala zima la mapenzi si chini
ya miezi mitatu na hii itaipa akili yako kusahau yaliyopita na kufungua
ukurasa mpya katika swala zima la mapenzi.
Baada ya kukaa
kipindi cha miezi mitatu sasa unashauriwa kuanza kutafuta mpenzi mpya
ambaye unaamini hata kutenda kama wa mwanzo, ina unashauriwa kuhakikisha
hurudii makosa uliyoyafanya mwanzo.
Jambo la tatu ni
kuhakikisha unakamilisha tathimini ya mapenzi. Hii ina maana ya
kujitathimini upya kama una kasoro ambazo ni kikwazo katika mapenzi.
Mathalani, ukali uliopitiliza, uchoyo, ukosefu wa huruma kwa mpenzi
wako, kiburi na roho ya wivu usiokuwa na tija!
Waswahili
husema, mke hapigwi kwa kofi au gondo/fimbo, bali mke hupigwa kwa
khanga, vivyo hivyo kwa mpenzi. Hakikisha unakuwa mpenzi ambayo
unavutia wakati wote, usiyechokwa kwa namna yoyote.
Unatakiwa
kuwa na saikolojia ya hali ya juu ya kutambua tabia za mpenzi wako, nini
anachotaka, wakati gani na kwa kutambua hayo ni rahisi kuishi katika
mapenzi yenye raha wakati wote.
Vijizawadi havitakiwi kukoma
kwa mpenzi wako, lakini hakikisha ni zawadi ambayo mpenzi wako anaipenda
baada ya kuwa umefanya saikolojia ya kile anachopenda.
Kumekuwa na fikra miongoni mwa watu kuwa mpenzi wa kike hawezi
kumnunulia zawadi mpenzi wake, lahasha; ukweli ni kwamba hata mpenzi wa
kike huweza kumnunulia zawadi mpenzi wake, na hayo ndiyo mapenzi ya
kweli.
on Thursday, 16 July 2015
Post a Comment