Tangu mbio za Urais zianze kushika kasi mkurugenzi wa IPP Media ndugu
Regnald Mengi alionekana wazi wazi kuiunga mkono timu ya UKAWA
Ghafla Mkurugenzi huyo ameamua kujitoa kwenye timu hiyo baada ya kuona
anapoteza nguvu zake wakati ana uhakika wa 100% kuwa Magufuli ndiye Rais
wa awamu ya tano. Mengi amesema haoni faida ya kupoteza muda wake
kumuunga mkono mtu mwenye uhakika wa kushindwa. Mengi amekubali wazi
kuwa ushindi wa kiti cha Urais 2015 ni wa Magufuli... "kama hawa jamaa
watashinda nafasi ya Urais basi ni baada ya miaka 10 siyo hivi sasa, huu
mwaka ushindi utakuwa wa Magufuli tu tutake tusitake"
Pigo kubwa kama hilo limeambatana na kuondoka kwa wasanii mbalimbali
waliotimkia kambi ya Ndugu Magufuli akiwemo Aunt Ezekiel, Ray na Juma
Nature. Mshirika wake mkuu Hussein Bashe nae amejiweka pembeni na
kuutangazia umma kuwa "ili wananchi wawe salama ni lazima kiti cha urais
kikabidhiwe kwenye mikono salama, kinyume chake wananchi hawatokuwa
salama, na mikono salama ni ya ndugu Magufuli tu"
Mwaka wa kufa nyani miti yote huteleza, EDO keshaanza kufa na miti yake pia imeanza kuteleza taratibu
Loading...
Post a Comment