Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

Mama Amchoma Mwanaye Kwa Maji Moto Baada ya Kumtuhumu Ameiba Nyama Jikoni

Polisi mkoa wa Mara inamshikilia mwananke mmoja (jina tunalo) mkazi wa Bweri Manispaa ya Musoma kwa kosa la kumchoma mtoto wake mwenye miaka minne, kwa maji ya moto, mikono yote miwili baada ya kumtuhumu kuwa ameiba nyama jikoni.

Mama huyo alikamatwa Novemba 14 saa nne asubuhi katika eneo la Morembe kata ya Bweri mjini Musoma baada ya Polisi kufika nyumbani kwake kumkamata kwa kosa jingine la kumkatakata kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili Kabula Rubeni (32) akimtuhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mume wake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, ACP Alex Philip Kallangi alidai kuwa siku ya tukio hilo la kumchoma moto mtoto huyo, mama yake mzazi alikuwa amepika nyama jikoni na baadaye alikwenda kuchota maji.

Kamanda Kallangi alidai baada ya mama huyo kurudi alimkuta mwanaye anakula nyama ndipo alishikwa na hasira na kuanza kumchapa sehemu mbalimbali za mwili wake na kisha akachukua mikono yote miwili na kumchoma kwa maji ya moto.

Baada ya kufanya kitendo hicho cha kinyama, mama huyo alianza kumtibu mtoto huyo kwa siri hapo nyumbani kwa dawa za kienyeji bila majirani kufahamu kilichokuwa kikiendelea nyumbani kwa mama huyo.

Kamanda Kallangi alieleza kuwa kilichosababisha kufahamika kwa taarifa hizo, ni baada ya Kabula aliyekuwa ameshambuliwa kwa mapanga na mwanamke huyo kwenda polisi kutoa taarifa ya kushambuliwa.

Kallangi alieleza kwamba polisi walipofika nyumbani kwake ndipo walipewa taarifa za mtoto huyo kujeruhiwa kwa kuchomwa moto. Kutokana na tukio hilo polisi hao, kwa kushirikiana na maofisa ustawi wa jamii na kituo cha ushauri cha Jipe Moyo walimchukua mtoto huyo na kumpeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara kwa matibabu na kisha kupelekwa Jipe Moyo anakoishi hadi sasa kwa uangalizi zaidi.

Kallangi alisema mtuhumiwa huyo yupo kituoni na anatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni kujibu mashtaka yanayomkabili.

Ofisa Ustawi wa Jamii Musoma, Vedastus George aliwataka wazazi na walezi kuzuia hasira zao pale watoto wanapowakosea na hata wanapowaadhibu wawe makini ili waziwaumize kama alivyofanyiwa mtoto huyo.

Lowasa Ajikanyaga kanyaga Alipokua Akihojiwa na Zuhura Yunus wa BBC Swahili

Siasa zetu za hapa kwetu ambazo wakati mwingine wanasiasa wanawaandaa waandishi wa habari ili wawaulize maswali yakuwapendelea leo imekua tofauti baada ya mh Lowasa kukutana na maswali ya BBC na Kuyajibu juu juu bila kuingia kwa undani zaidi:

BBC:Mh Lowasa unasema kwamba utatoa elimu bure kuanzia chini mpaka chuo kikuu hizi pesa zitapatikana vp?
Jibu:Pesa zipo nyingi tu kwenye gesi,tuna madini....!
BBC:Lakini ulishakua waziri mkuu vp hili lilishindikanaje ukiwa waziri mkuu?
Jibu:Tulijenga shule za kata nyingi sana.
BBC:Lakini elimu haikua bure mh Lowasa?
Jibu:Nadhani unanionea.
mmmmmh!
Kesho atahojiwa Magufuli ndipo watu watatofautisha hawa wawili.
Kimsingi Lowasa ka fail kukutea hoja zake na jibu ni raisi tu kwamba hizi ni ahadi zisizotekelezeka ndio maana anashindwa kujieleza sawasawa.

Ujumbe wa Paul Kagame kwa Jakaya Kikwete, ni Mtihani Kwa CCM

UJUMBE MUHIMU WA KAGAME KWA JAKAYA KIKWETE KUELEKEA UCHAGUZI MKUU!!

"Kuhubiri kuhusu demokrasia ni jambo moja na kusimamia demokrasia ni jambo jingine!!Kama Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki tunafuatilia yale yanayoendelea Tanzania wakati ikielekea katika Uchaguzi wao Mkuu; hivyo tuna hamu ya kuona rafiki yetu na Mwenyekiti wetu anayesimamia jumuiya yetu akithibitisha kwetu namna demokrasia inavyotakiwa kusimamiwa kwa vitendo nchini Tanzania ili ajitofautishe nami ama na Nkurunzinza"...Kagame, Paul....


Je unakubaliana na Paul Kagame kwa niaba ya Viongozi wenzake wa Afrika Mashariki? Unadhani Jakaya Kikwete anatakiwa kuwathibitishia namna gani demokrasia inavyotakiwa kutekelezwa hapa Tanzania?..Je kunaviashiri vyovyote vya demokrasia kuvunjwa na haki kuzimwa chini ya Usimamizi wa Jakaya Kikwete?..Usiogope TIRIRIKA!!

Alichokiandika Zitto Kuhusu Rafiki Yake Deo Filikunjombe


Lowassa: Wananchi Anzeni Kusherekea na Kushangilia Ushindi

Huku zikiwa zimebaki siku 13, Mgombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendelea na anayeungwa mkono na umoja wa Ukawa Ndg. Edward Lowassa kawataka wananchi waanze sasa kushangilia ushindi na ukombozi wa pili wa Taifa hili.

Lowassa kasema hayo jana alipokuwa mjini Musoma, ambapo alipata mapokezi ambayo hayajawahi kutokea, tokea nchi ipate uhuru. Lowassa kasema kutokana na mapokezi na hamasa kubwa ya vijana, wakina mama, na wazee anayopata, kawataka wananchi waanze kushangilia ukombozi wa pili unaotarajiwa kutokea oktoba 25.

Lowassa kasema baada ya oktoba 25, kila mwananchi ataanza kufaidika na matunda ya mgao wa keki ya Taifa, na sio hali ilivyo ya sasa, ambapo keki inamegwa na wachache na kuacha vijana wengi, bodaboda, machinga, wakina mama vijijini, walimu, madaktari, wafanyabiashara, wauguzi, wakulima na wafugaji wakiwa hawana hata uwakika wa kupata milo mitatu. Hilo linakoma mara moja baada ya oktoba 25..

"najua uhuzi, masikitiko na mfadhaiko mliyonayo wananchi. Mwisho wa hayo yote ni tarehe 25, ndio maana nataka muanze kusherekea kuanzia sasa kwani naenda kuwatoa kwenye kifungo cha kunyimwa fursa na serikali ya CCM kwa zaidi ya miaka 54"...

Vile vile kawataka wananchi kwa uwingi wao siku ya tarehe 25.10.2015 wajitokeze kwa wingi sana sana kupiga kura...

Ulishawahi kuona mlo wa mchana wa Cristiano Ronaldo? basi nimekuwekea hapa mtu wangu


Michuano ya mechi za kuwania kufuzu michuano ya Euro 2016 bado inaendelea kwa michezo kadhaa kupigwa, kwa upande wa timu ya taifa ya Ureno ambao walishinda kwa goli 1-0 dhidi ya timu ya taifa ya Denmark . Baada ya ushindi huo Ijumaa ya October 9 Cristiano Ronaldo alipiga picha za mlo wake wa mchana.
Cristiano Ronaldo alipost picha ya msosi wake wa mchana aliyokula wakati ambao alikuwa anajiandaa kurudi kwao ni diet ambayo imekamilika kwa kiwango kikubwa, kwani kulikuwa na mayai, viazi, nyama, matunda, maji ya kunywa juisi. Baada ya kuweka picha hiyo katika account yake ya instagram mtandao wa dailymail.co.uk ulichambua kila aina ya chakula kilichomo katika diet hiyo.
 Katika ratiba ya chakula cha mchana cha Ronaldo hakuna chakula ambacho kina asili ya sukari nyingi lengo linatajwa kuwa ni kulinda mwili wake ili kuendelea kuwa sawa kwa michuano mingine. Ureno walicheza mechi dhidi ya Denmark na kuibuka na ushindi wa goli 1-0, huu ukiwa ushindi wao wa sita katika mechi zao saba za kuwania kufuzu michuano ya Euro 2016.

Magufuli Azomewa Jijini Mbeya.....Wananchi Wasema Wanamtaka Lowassa. Hapa kuna Video Mbili


Katika  hali  isiyo  ya  kawaida,Mgombea  Urais  kwa  tiketi  ya  CCM, Dr. John Magufuli  leo  alijikuta  katika  wakati  mgumu  baada  ya  kukutana  na zomea zomea  ya  kundi  la  vijana  waliovamia  msafara  wake  akiwa  njianI  kuelekea  Mbarali  na kuanza  kuimba wakidai  Lowassa  ndo  Rais  wao

Pamoja  na  kadhia  hiyo,Magufuli  alifanikiwa kufika  Mbarali  na  kuhutubia  maelfu  ya  wananchi  ambao  amewaahidi  kushughulikia  migogoro  yao  ya  muda  mrefu  ambayo  imekuwa  kete  ya  kuombea  kura  kwa  baadhi  ya  wanasiasa  wenye  uchu  wa  madaraka

Dr. Magufuli  leo  pia  amefanya  mikutano  kadhaa  ya  kampeni  mkoani  Iringa  ambako  alilazimika  kumalizia  viporo  hivyo vilivyokuwa  vimebaki  mkoani  humo. 

Total Pageviews

Powered by Blogger.
Menu :

Featured Posts

© Copyright AMSHA EVENTS | Distributed By Blogspot Templates
Back To Top