Huku zikiwa zimebaki siku 13, Mgombea wa Chama Cha Demokrasia na
Maendelea na anayeungwa mkono na umoja wa Ukawa Ndg. Edward Lowassa
kawataka wananchi waanze sasa kushangilia ushindi na ukombozi wa pili wa
Taifa hili.
Lowassa kasema hayo jana alipokuwa mjini Musoma, ambapo alipata mapokezi
ambayo hayajawahi kutokea, tokea nchi ipate uhuru. Lowassa kasema
kutokana na mapokezi na hamasa kubwa ya vijana, wakina mama, na wazee
anayopata, kawataka wananchi waanze kushangilia ukombozi wa pili
unaotarajiwa kutokea oktoba 25.
Lowassa kasema baada ya oktoba 25, kila mwananchi ataanza kufaidika na
matunda ya mgao wa keki ya Taifa, na sio hali ilivyo ya sasa, ambapo
keki inamegwa na wachache na kuacha vijana wengi, bodaboda, machinga,
wakina mama vijijini, walimu, madaktari, wafanyabiashara, wauguzi,
wakulima na wafugaji wakiwa hawana hata uwakika wa kupata milo mitatu.
Hilo linakoma mara moja baada ya oktoba 25..
"najua uhuzi, masikitiko na mfadhaiko mliyonayo wananchi. Mwisho wa hayo
yote ni tarehe 25, ndio maana nataka muanze kusherekea kuanzia sasa
kwani naenda kuwatoa kwenye kifungo cha kunyimwa fursa na serikali ya
CCM kwa zaidi ya miaka 54"...
Vile vile kawataka wananchi kwa uwingi wao siku ya tarehe 25.10.2015 wajitokeze kwa wingi sana sana kupiga kura...
Loading...
Post a Comment