Umoja wa Ulaya (EU) umeishtaki rasmi kampuni ya Google kwa matumizi mabaya ya soko lake kufuatia uchunguzi uliofanyika kwa miaka mitano.
Kamishna wa ushindani katika umoja huo wa Ulaya Margrethe Westager amesema jana kuwa ana wasiwasi kwamba kampuni hiyo ilikuwa na upendeleo ambapo ni kinyume na sheria zake za uaminifu.
Pia ilianzisha uchunguzi kuhusu mfumo wa Android katika kampuni hiyo.
Kampuni hiyo ya mtandao imeomba zaidi ya miezi miwili ili kujibu mashtaka hayo yanayoikabilia.
Hata hivyo hakuna tamko lolote lililotolewa na kampuni ya Google kuhusu tuhuma hizo na huenda wakapigwa faini.
Post a Comment