Umakini katika maisha ya uhusiano ni mzuri, kwanza kutakujenga
kiakili, moyo hautakuwa na ukakasi maana una msimamo thabiti. Suala la
kupenda ni muhimu.
Unaweza kupendwa lakini usipende. Unaweza kuwa na mwenzi wako ambaye
mmefunga ndoa kabisa, lakini usiwe na mapenzi naye au pendo likapungua
na baadaye kuyeyuka kabisa.
Hifadhi pendo moyoni mwako. Penzi ni uwekezaji. Lazima uwekeze pendo
moyoni mwako, ujifunze kuwa katika uhusiano sahihi ili siku zijazo
uyafurihie maisha.
Mapenzi hayatakuwa na maana kwako kama huna uwezo wa kupenda. Faragha
haitakuwa na maana kwako kama hutakuwa na hamu na tendo lenyewe. Wengi
wana tatizo hili lakini hawajajua namna ya kujitibu.
Wengi huona ufahari kuwa na wenzi wengi lakini athari zake
kisaikolojia ni kubwa. Mahodari wa wenzi wengi hupoteza uwezo wa kupenda
na hamu ya tendo.
Hujawahi kuona baba/mama mtu mzima kabisa, mweye miaka zaidi ya 50
bado anafukuzana na dogodogo? Unadhani anatafuta nini alichokosa kwa
mwenzake? Si kweli kwamba mwenzake hana uwezo kama zamani.
Ni athari ya kutotosheka. Kama mtu umempenda, hata akizeeka, mnazeeka
pamoja. Mnalandana kwa kila kitu kwahiyo hata mapenzi nayo huongezeka
zaidi. Kuona watu wazima wakikimbizana na watoto huko nje, maana yake ni
wagonjwa! Wameshaathiriwa na mfumo mbaya huko nyuma.
TAFITI MWENYEWE
Fanya uchunguzi mdogo utagundua kuwa, hata hao
watu wazima wenye wapenzi ‘dogodogo’ huwa hawawezi kuwa na mmoja tu. Leo
huyu, kesho yule! Ni kwa sababu anaumwa na anajaribu kutafuta tiba
ambayo si sahihi kwa hakika.
Tiba yake ni ushauri tu. Akalishwe chini na kuelezwa anapokosea ni wapi na kumtengeneza ‘mtu’ mwingine kichwani mwake.
USHAHIDI
Utafiti unaonyesha kuwa, mtu aliyepata kuwa katika
uhusiano na wenzi wengi hupoteza uwezo wa kupenda. Yaani anakuwa na mtu
leo akiamini kuwa amempenda lakini akishakutana naye faragha anajikuta
hamu ya kuwa naye imetoweka!
Wengi kuanzia hapo wanaanza kuwachukia. Tabia hiyo huota mizizi na kujikuta kila wakati akiingia katika uhusiano mpya.
LADHA HUONDOKA
Aidha, mtu ambaye amezoea kukutana na mapatna
wengi, hupoteza hamu au kukosa ladha ya tendo. Watu wa namna hii,
hujikuta wakiwajua watu wa jinsi pacha ‘sana’ kiasi cha kuanza kuwa
wakaguzi mno na mwishowe hamu au ladha hupungua kama siyo kupotea
kabisa.
Mariam (si jina halisi) mkazi wa Sinza, Dar ni mwanandoa. Ana miaka
34. Ana watoto wawili na mumewe ambaye ni mwajiriwa serikalini. Alifika
ofisini wikiendi iliyopita kunitaka ushauri.
Alisema: “Mume wangu amenizidi umri kidogo, yeye ana miaka 44.
Anatunza familia yake vizuri. Mimi na watoto tunaishi vizuri lakini
tatizo huyu bwana ni mhuni sana. Yaani asione mwanamke mbele yake.
Kishatembea na mahausigeli zaidi ya wanne, nikaamua kumleta ndugu yangu,
naye akalala naye.
“Ni mwanaume nisiyemwelewa kabisa. Hilo linanifanya nikose amani na
ndoa yangu, maana hata faragha anakuwa goigoi. Anajijali mwenyewe, yaani
ndoa naiona chungu.”
Baada ya mazungumzo marefu na kumwuliza vizuri kuhusu historia yao ya
uhusiano, ilionyesha kwamba mumewe ana tatizo hilo la kupoteza uwezo wa
kupenda na kukosa hamu ya tendo. Nilimaliza kesi yake vizuri.
Inawezekana nawe una tatizo kama hilo lakini hujui namna ya kujiondoa, wiki ijayo tutaendelea, USIKOSE!
Loading...
Post a Comment