Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu, amesema chama chao
kinatarajia kupata wanachama wengi baada Waziri Mkuu mstaafu, Edward
Lowassa kujiunga na chama hicho.
Lissu ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo taarifa kwamba wapo
wanachama wa CHADEMA ambao watakihama chama hicho kutokana na
kutokubaliana na ujio wa Lowassa ndani ya CHADEMA.
Akizungumza jana na waandishi wa habari Lissu alisema,
“Kama wapo watakao jiondoa CHADEMA, wengi zaidi
watakuja. Tupo katika kipindi ambacho hatujawahi kuwepo tangu mfumo wa
vyama vingi uanze. Mfumo tawala unabomoka vipande vipande. Unapobomoka,
dalili zake ni watu ambao wamekuwa katika mfumo huo kuondoka kama
alivyofanya Lowassa.”
“Mabadiliko katika nchi yanatokea pale mfumo tawala unapo pasuka. Lowassa ni mfano mzuri.
"Tunamkaribisha kwetu siyo kwa sababu ni mwanasiasa
msafi. Tumempokea kwa sababu tunaongeza nguvu kubwa kwa wale wanaotaka
mabadiliko. Imetokea Zambia Mawawi, Nigeria na Kenya”
Akizungumza kuhusu CHADEMA kumtuhumu Lowassa kwamba “ni fisadi” kabla ya kujiunga na chama hicho Lissu alisema;
“…hatukuwa na makosa hata kido kumweka Lowassa katika
kundi la watuhumiwa wa Richmond. Mambo yalizungumzwa bungeni.
Aliwajibika na amesema mwenyewe aliwajibika.”
“Alijiuzulu Uwaziri Mkuu kwa sababu ya Richmond.
Tulimweka katika orodha ya mafisadi kwa sababu ya Richmond. Na jana
alisema alimwambia rais “tuvunje mkataba” rais akaataa. Angefanyeje?
Hilo ni vumbi, litakapotulia Chama Cha Mapinduzi na mfumo tawala utakuwa
umeanguka, tutajenga nchini. Bila kuvunja mfumo tawala hakuna kusonga
mbele,”
Post a Comment