Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

SABABU ZA WANAUME KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA

Natumai utakuwa u mzima wa afya kabisa. Kama ilivyo matatizo mengine tatizo la kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa huwakumba na wanaume vilevile ila siyo kwa kiwango kikubwa sana kama ilivyo kwa wanawake.
Katika makala haya tutaaangalia kwa kina sababu za tatizo hili kwa wanaume na athari zake na mwisho tutajifunza njia za kutatua au kuondokana na tatizo hili.
Mwili wa mwanadamu uliumbwa ukiwa na matamanio na si mbaya kama mwenye mwili atakuwa na uwezo wa kujitawala. Wanaume wengi huvutiwa zaidi na hisia za kushiriki tendo kwa kuona baadhi ya maungo ya wanawake, kusikia sauti na hata migusano.
Kuna wanaume wengi wao wapo tu siku zinaenda hawapati hamu ya kushiriki tendo la ndoa na wanajiona kama ndiyo wamefanikiwa kujitawala kumbe ni wagonjwa.
Habari njema ni kwamba pamoja na tatizo hili kuwasumbua watu wengi kuna mambo unayoweza kuyafanya kupunguza ukubwa wa tatizo hili au kuliondoa kabisa, kwa kutumia mimea tiba na matunda tiba.
Unachotakiwa kufanya kama umejaribu kutumia njia mbalimbali ili kuondoa tatizo hili bila mafanikio basi wahi mapema kwa wataalamu ufanyiwe uchunguzi au ukatutembelea Sigwa Herbal Clinic tukakusaidia kuliondoa kabisa tatizo hilo na ukarejea katika hali ya kawaida.

Baadhi ya watu wanaamini kuwa hamu ya kufanya tendo la ndoa inapungua kadiri umri wa mwanaume unavyoongezeka. Kuna idadi kubwa tu ya wanaume ambao hamu yao ya kufanya tendo la ndoa imebaki vilevile hata umri wao ulipokuwa mkubwa kabisa. Kwanza tuanze kwa kutazama ukubwa wa tatizo hili.
Idadi ya wanaume wanaoridhika kuishi na tatizo hili ni ndogo sana ukilinganisha na ile ya wanawake.
Hata hivyo, tatizo la mwanaume kukosa hamu ya kushiriki tendo limekuwa ni chanzo kikubwa katika kuleta migogoro katika ndoa nyingi.
Wanaume kwa kawaida ni wabishi sana na huwa hawapendi kuaibika hivyo mtu anaweza akawa na tatizo ila hapendi mwenzi wake ajue kama ana tatizo ambalo kumbe angeliweka bayana angepata ushauri wa namna ya kulitatua.
Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana

Total Pageviews

Powered by Blogger.
Menu :
© Copyright AMSHA EVENTS | Distributed By Blogspot Templates
Back To Top