Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

Hii ndio sababu iliyomfanya Justin Bieber adondoshe machozi kwenye usiku wa MTV VMA’s 2015.

Baada ya kuweka headlines nyingi usiku wa tuzo za MTV VMA’s mwaka huu na show iliyoisha kwa machozi, Justin Bieber kaamua kuzungumza sababu zilizompelekea kuangusha machozi akiwa katikati ya show yake  ya MTV VMA’s 2015 jijini Los Angeles Marekani.
Siku ya Jumatano msanii huyo wa R&B Pop alialikwa kwenye kipindi cha ‘The Tonight Show’ cha Jimmy Fallon kuzungumzia maisha yake,video yake mpya pamoja na tukio lililotokea usiku wa MTV VMA’s siku ya jumapili August 30.





>>“Nilifurahi kupita kiasi, nimefanya utoto mwingi hapa kati kati na wala sikutegemea kama watu wangeonyesha support kubwa sana kwangu siku ile kwa sababu mara ya mwisho mimi kuperform kwenye show nilizomewa sana nikajisikia vibaya”. <<< Justin Bieber.
Justin Bieber alikiri kuwa alikuwa mkorofi bila sababu za msingi, aliwakwaza wengi na alichukulia vitu vingi sana poa kiasi cha yeye kusahau tarehe ya uzinduzi wa moja ya album zake hivyo alihisi kuwa akirudi jukwani watu hawatampokea vizuri na pengine wengi wanamchukia.
Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana

Total Pageviews

Powered by Blogger.
Menu :
© Copyright AMSHA EVENTS | Distributed By Blogspot Templates
Back To Top