Lowassa na Magufuli
Vyama vyote vya siasa vimekubali kufanya mdahalo wa wagombea wa Urais
kwenye vyombo vya habari lakini vyama vinavyounda UKAWA vimekataa
kushiriki kwenye midahalo hiyo kwa kutoa sharti moja la kutomshirikisha
mgombea wao na badala yake waende wenyeviti wa vyama.
Utaratibu wa dunia nzima kwenye midahalo wanahudhuria wagombea na siyo
wenye viti wa vyama... Yaani Rais Kikwete aache majukumu yake ikulu
halafu aende kwenye vyombo vya habari kufanya midahalo wakati kwenye
midahalo wanazungumzia sera za chama husika na sasa aliyebeba sera za
CCM ni Ndugu Magufuli.
Baada ya kufanya uchunguzi sababu zifuatazo zimebainika kuwa ndiyo
vigezo vya kumfanya mgombea wa UKAWA ndugu Lowassa kususia midahalo hiyo
1. Afya yake ni dhaifu na haimruhusu kukaa muda mrefu bila kupewa dawa
ya kumuongezea nguvu. kwenye mikutano yake ya kampeni hajawahi
kuzungumza zaidi ya dakika 15, sasa atawezaje kuhudhuria mdahalo
akaongea zaidi ya nusu saa?
2. Amehusika sana kwenye kashfa nyingi za ubadhilifu wa mali za umma na
hana uwezo wa kukataa ukweli huo, hata alipoulizwa na waandishi wa
habari huko Dodoma alikataa kulijibu hilo swali, na endapo atahudhuria
kwenye mdahalo wowote hilo swali hawezi kuliepuka
3. Chama chake hakina sera nzuri, anakosa kitu cha kuongea awapo mbele
ya watu kwakua chama chake hakijaandaa ilani nzuri yenye sera za
kumkomboa Mtanzania. Wakati wenzake wanatoa sera za kupunguza gharama za
ujenzi yeye anamwaga sera za kuwatoa jela akina Babu Seya na kubomoa
nyumba za nyasi nchi nzima kwa muda wa siku 100
Loading...
Post a Comment